Sunday, 25 August 2013

 KUHUSU RASIMU YA KATIBA MPYA TANZANIA 2013.
 N i wazi kuwa kira raia wa Tanzania na asiye wa Tanzania anjua kuwa  Tanzania imeungana na nchi nyingine katika mabadiliko ya katiba. mataifa mengi ya afrika na amerika kusinii na caribian zimekuwa katika hali ya kubadilisha katiba zao ili ziiendane na demokrasia magharibi.

katika michakato ya katiba kuna vitu vingi vinavyotokea mfano wananchi kutoa maoni yao, kupitia katiba ya zamani,  kuangalia katiba za watu wengine n.k.

tukumbuke kuwa rasimu yetu ya katiba imechukua baadhi ya vifungu kutokanan na maoni yetu na vingine kutoka katiba na rasimu za wezentu hasa ile ya kenya ya 2010 ambayo ndiyo imesimamia  uchaguzi wa Kenya ulioisha.

katiba yetu ya mwaka 1977, ilikuwa haina kifungu kinacho ruhusu matokeo ya uraisi kuhojiwa mahakamani baada ya kutangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi. jambo hili lililamikiwa kwa muda mrefu n wanaharakati na hatimaye rasimu hii ya 2013 imeweka kifungu kinacho ruhusu hilo.

lakini mbali na kuweka kifungu hicho bado kina mapungufu y kimsingi yanyokifanya kifungu chenyewe kutokuwa na maana. kwani kinatoa haki upande mmoja na kinany'anganya  haki upande mwingine. kifungu hiki bali na maoni ya wannchi, msingi wake mkubwa ni rasimu ya kenya ya mwaka 2010. yenye kifungu kama hicho.
ukisoma rasmu ibara ya 78 (1) inasomeka hivi "kwa kuzingatia masharti ya ibara ndogo ya (2), endapo mtu yeyote aliyeshiriki kama mgombea nafasi ya madaraka ya Rais katika uchaguzi wa Rais hakuridhika na matokeo ya uchaguzi huo anaweza kuwasilisha malalamiko katika Mahakama ya juu kupinga matokeo ya Rais yaliyotangazwa na tume huru ya uchaguzi."

              (2) malalamiko ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais yatawasilishwa mahakama ya juu ndani ya muda wa siku saba baada ya siku ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Rais.

79 (1)Rais mteule ataapishwa na Jaji mkuu na atashika nafasi ya madaraka ya Rais mapema iwezekanavyo baada ya kutangazwa kwamba amechaguliwa kuwa Rais, lakini kwa hali yoyote hatashika madaraka kabla ya kupita siku thelathini kutoka siku matokeo ya uchaguzi wa Rais yalipotangazwa na Tume Huru  ya Uchaguzi au siku ya kuthibitishwa na  Mahakama ya Juu.

ukisoma vizuri vifungu hivi utaona kabisa kimoja kinauliwa na kingine na hasa cha 78 hakina nguvu yeyote dhidi ya kifungu cha 79, kwani hakijatoa muda kwa watu au mtu mwenye lalamiko juu ya matokeo. raisi akishaapa tiyari atakuwa ameshika madaraka na kuwa raisi pia. 

na kama tutaacha kifungu cha 79 kiendelee kusomeka kama kilivyo basi tutategemea sana busara za viongozi wa tume ya uchaguzi. 

kifungu hiki tume kitoa kenya na katiba ya kenya inaonyesha vizuri na imeweka siku za kuapishwa sio kutangazwa na kuaapa.

soma  kifungu cha 140 na 141 cha katiba ya kenya hapo chini.
 
 Ibara ya 140. Maswali kama uhalali wa uchaguzi wa rais

(1) Mtu anaweza kuwasilisha malalamiko katika Mahakama Kuu kupinga uchaguzi wa Rais mteule ndani ya   siku saba baada ya tarehe ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi wa rais.
(2) Ndani ya siku kumi na nne baada ya kufungua jalada la malalamiko hayo chini ya kifungu cha (1), Mahakama Kuu itasikiliza na kuamua malalamiko na uamuzi wake utakuwa wa mwisho.
(3) Kama Mahakama Kuu huamua uchaguzi wa Rais mteule kuwa batili, uchaguzi mpya utafanyika ndani ya siku sitini baada ya uamuzi.

Ibara ya 141. Kushika madaraka ya Rais
(1) kuapishwa kwa Rais mteule-watakuwa katika umma mbele ya Jaji Mkuu, au, kutokana na kukosekana kwa Jaji Mkuu, Naibu Mkuu wa Sheria.
(2) Rais mteule-ataapishwa juu ya yafuatayo kwanza Jumanne -
        (A) siku ya kumi na nne baada ya tarehe ya tangazo la matokeo ya uchaguzi wa rais, kama hakuna malalamiko imekuwa filed chini ya Ibara ya 140; au
        (B) siku ya saba baada ya tarehe ambayo mahakama mithili uamuzi kutangaza uchaguzi kuwa halali,       ikiwa dua yoyote imekuwa filed chini ya Ibara ya 140.
(3) Rais mteule kushika madaraka kwa kuchukua na subscribing kiapo au uthibitisho wa utii, na kiapo au tamko la dhati kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu ya ofisi, kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Tatu.
(4) Bunge na sheria kutoa kwa ajili ya utaratibu na sherehe kwa ajili ya kuapishwa kwa Rais mteule.

ndugu zangu naomba mlinganishe vifungu hivi.