
katika mambo makubwa ambayo kimsingi Watanzania hatutayasahau ni "imani na matendo" ya Mwalimu Nyerere wakati wa uhai wake na katika mambo yote aliyo yaandika wakati wa uhai wake. Mwalimu Nyerere amekuwa katika wanafalsafa, wasomi na wanasiasa wa ulimwengu huu ambao imani yao ilikuwa katika "usawa", "haki" "umoja na mshikamano". Mwalimu Nyerere hakupenda unyonyaji hivyo hakutenda matendo hayo, alichukia sana rushwa mpaka kiasi cha kuamua kuvunja sheria alipo tunga sheria ya kuwachapa viboko wala rushwa na watoa rushwa akihutubia Mwalimu Nyerere alisema"mtu akila rushwa, akipokea rushwa, aliyetoa, aliyepokea wazanaki wanasema wote mazaganyanza, wote watapata misukosuko........ akisha kuthibitika mahakamani kwamba katoa rushwa, kwamba kapokea rushwa, hatukumuachia hakimu uamuzi wa hadhabu tukasema atakwenda dani kwa muda husiopungua miaka miwili, atapata viboko ishirini na vinne, kumi na viwili siku anaingia na kumi na viwili siku anatoka akamuonyeshe mkewe" .

Mwaka 1964 alishirikianan na Watanzania wengine katika harakati za kuunganisha Tanganyika na Zanzibar ilikuwa na nchi moja yenye nguvu.
Matendo yake hayo na imani ya usawa na haki na amani, mwaka 1967 alianzisha "siasa ya ujamaa na kujitegemea", lengo lake kubwa likiwa ni kutaka mgawanyo sawa wa raslimali za nchi kwa wananchi wote wa Tanzania. Pia siasa hiyo ililenga kuondoa mazingira ya ukandamizwaji, unyonywaji na udhalilishwaji wa binadamu. Mwalimu aliamini kuwa binadamu wote ni sawa. Imani ya TANU ya kwanza ilitamka kuwa "binadamu wote ni sawa" na ya pili ilisema kuwa "kwamba kila mtu anastahili heshima"
Mwalimu Nyerere katika hotuba aliyoitoa mwaka 1967 kwa wanachuo wa chuo cha ualimu Chang'ombe alisema kuwa " binadamu wote ni sawa .......basi lazima tukubali kwamba kunyonywa na kudhaliwa kwa binadamu mahali popote ni kuonewa, kunyonywa, na kudhiliwa kwa binadamu wote. binadamu wote wanapunguzwa utu wao kwa uovu wao" Maneno haya yanamdhihirisha Mwalimu Nyerere alikuwa mtu wa aina gani. Hukiona au kusikia hivi je unapata swali gani. nadhani swali la kwanza linalojitokeza ni nani anaishi maisha haya kwa sasa?
swali hili linaweza kujibiwa kwa kunyosheana vidole au kujinasibisha na Mwalimu Nyerere, kwa midomo tu na kushindwa kutenda. Kwa sasa tukizungumza mambo ya rushwa utaona rushwa zipo mpaka hadi watu wake wa karibu, unyonyaji na unyanysaji , ukandamizaji yote haya yanatendwa na wale ambao kwa wakati mwingine watanzania na dunia nzima haiamini kuwa wanatenda hivyo.
hakuna mtu anaweza kumunyoshea Mwalimu Nyerere kuhusu suala la kuheshimu utu wa mtu. lakini sasa watu wengi walitegemea zao lake lingeendeleza utu na usawa wa binadamu.
tukiangalia matendo ya viongozi wetu wa kisiasa, kidini, kijamii na makazini huko tunakoishi tunashuhudia kabisa vitendo vya ukandamizaji, unyonyaji, udhalilishwaji na mengine mengi.
tunabudi watanzania tujitathimini na kujiuliza ni wapi tumekosea na tunahitaji kukosoa nini ili tutende yale tuliyoelekezwa na Mwalimu Nyerere. tanzania inanuka rushwa, matabaka na umaskini.