Thursday, 11 July 2013

HIVI NINI MAANA YA GREEN GUARD?

Napata shida sana na matamshi ya Mh JK ( raisi wetu), aliyoyatoa siku ya maazimisho ya miaka 50 ya JWTZ. raisi alikemea na kusuta watu wano andaa au vyama vya siasa vinavyo jipanga kufanya mafunzo ya mgambo kwa vijana wao? 

suala hili kwa tafsiri ya haraka haraka tunaweza kusema mhe Raisi anataka kuondoa shida ya kuja kuwa na majeshi ya waasi hapa nchini . au kuwa na kile wataalamu wa masuala ya sasa wankiita sub state within a state, ambaloni jambo la hatari kwa taifa.

lakini ukijiuliza kwa kina unajiuliza kuwa mbona upande wake kuna kikundi kinachofanana na kile cha upande wa pili? lakini pia tumeshuudia katika vipindi vy achaguzi hapa nchini hawa grreen guard ndio huwa wanhusika katika ulinzi wa shughuli za chama chake, pili hwa green guard wamepatiwa semina mbalimbali za mafunzo ya mgambo ambao kimsingi yanatengeneza kikundi ambacho ni jeshi lachama japo kuwa halina silaha ila lina utaalamu.

suala la kujiuliza hapa ni je ni msingi hupi inaomfanya raisi akemee vyama vingine kuwa na vijana wa namna hii. na kama upande mwingine wapo, je hii inathibitisha maneno ya gazeti la mawio la mjini moshi  lilokifanananisha chama cha mapinduzi na utawala wa faraho? kwamba kwa chama tawala suala ni utawala tu hata kama unaweza au huwezi, au jambo lolote litapimwa usafi kulingana na upande linakotoka, mfano utakuwa huna kosa kuwa na vijana wanopewa semina za mgambo kama wewe ni CCM lakini litakuwa kosa kuwa na vijana wa namna hiyo kama wewe unatoka upande mwingine.

mimi sio mtaalamu sana wa mambo haya lakini haya nimeyaona na nimeona sio vyema nia yaache yapite bila kuyajadili kwa kina.

No comments:

Post a Comment