Thursday, 15 August 2013

MAMBO YA AMANI NA USALAMA WA TAIFA


Kuna mambo mabayao kimsiungi sikutaka kuyajadli ila nataka kuyajadili hii jioni, lakini kwa kuwa tiyari yameanza kujitokeza ni lazima niyaseme. hapa nchini tumekuwa na matatizo ya amani na usalama. na mambo haya yako katika ngazi ya taifa na kimataifa.

Hatari kwa taifa  (national threat) ni jambo ambalo laweza kuanzia ndani ya nchi au nje ya nchi , na ni wajibu wa nchi husika kujua kuwa iko katika hali ya hatari. hatari ya kutoka ndani inaweza kuundwa katika mazingira ya aina mbili moja inaweza kuundwa na vikundi vya waasi au wananchi wachache tu, na msingi  mkubwa wa vikundi hivi huwa kwa mara nyingi ni kutoridhika na matendo ya serikali au kikundi cha watu ndani ya serikali.
Wakati mwingine suala hili linaweza kuchochewa na serikali yenyewe bila kujua au kwa kujua. mfano serikali inaweza kuwabagua watu fulani kwa tofauti zao za kisiasa, kikabila , kiuchumi, kiimani na kikabila na kuwalazimisha kuunda kikundi. Kukiibuka kikundi kilichochowe na serikali basi hicho inakuwa ni vigumu mno kikigundua kwa sababu kinakuwa kinapigana na kikundi kingine bila kukilenga moja kwa moja. mfano mzuri ni vita ya Kongo au Biafra ya Naigeria ambapo serikali ilichochea tofauti za kidini kuanzia enzi za mkoloni na ikaja kuwa vita dhidi ya uislamu na ukristo lakini kupitia serikali.

wakati mwingine serikali inaweza kusababisha hili kwa kufanya ugaidi kwa watu wake mfano kuwateka na kuwapiga kuwaumiza, na katika mazingira kama haya serikali huwa inatumia sura ya kulinda amani na kuwalinda raia anowapiga. Hili limeanza kutokea hapa nchini. mtakumbuka kuwa bado kuna mvutano wa polisi na wanaharakati kuhusu suala la Daudi Mwangosi, Ndugu Absalom Kibanda, Dr Ulimboka, na sasa  Ndugu Ponda na mengine mengi.

Upande mwingine hatari ya taifa inaweza kutoka mataifa jirani na mengine ya nje. Taifa linaweza kuwa na marafiki ambao kimsingi wanaweza kuwa hatari kwa upande mwingine kulingana na mtandao wa itikadi na maslahi ya kiuchumi na kisiasa. mtakumbuka  suala la vita dhidi ya Ethiopia na Eriteria ambapo Amerika alijenga uadui na Misiri baada ya kusemekana kushirikiana na Israel kumsaidia Ethiopia dhidi ya Eritria.

lakini tusisahahu pia kuwa hata taifa husika linaweza kusababisha hatari kutoka nje, hali hii inaweza kutokea kupitia matamshi ya viongozi wakuu na wasimamizi wa serikali dhidi ya matifa mengine, au vyombo vya habari , mazoezi ya kijeshi mipakani n.k
 kwa hatua hii ebu nieleze suala hili kidogo kuhusu tanzania. hapa nchini kumekuwapo kumbukumbu nzuri ya watu kuvamiwa na kutekwa kunyanyaswa na pengine na watu wasio julikana lakini yakitokea hayo unasikia marumbano kati ya vyombo vya dola na makundi ya wanaharakti na wansiasa. lakini mbali na kuvutana huko hakuna siku umma wa Watanzania umeambiwa ukweli ni huu. tunabaki kujivicha kwenye ugaidi, udini na siasa tu.
leo niliposoma gazeti moja hapa nchini niliona likitaja kifo cah Prof Mwakusa ambaye alipigwa risasi muda mrefu kidogo na wanfunzi wa chuo kikuu na vyuo rafiki nchini waliaaandamanan wakitaka uchunguzi wa wauaji hao lakini mpaka sasa hakuna jibu. na kumbuka wakti huu nilikuwa mwanfunzi katika chuo hicho hivyo maneno yote yaliyo kuwa yanzungumzwa nilikuwa nayasikia na kuyaona.

lakini tunakumbuka kupigwa risaiasi kwa mwandishi wa habari Daudi Mwangosi, akiwa katika  shughuli zake za habari. Suala hili limeishia kukamtwa kwa kijana polisi mdogo na kufunguliwa mashitaka ya kumpiga risasi lakini ukiangalia mwennendo wa kesi unapata wasiwasi. ni sababu gani ya mtuhumiwa wa mauaji analindwa na serikali tena kwa kupigiwa ving'ora wakti akipelewkwa mahakamni na pengine kufungiwa misafara mirefu ya magari ya serikali hali kama hii inatia wasiwasi machoni pa watnzania.

tukio jingine nilile la kijana aliyepigwa risasi katika mkutano wa CHADEMA pale Morogoro. Serikali kupitia jeshi la polisi wakatwambia amepigwa na kitu kizito. lakini naye hatuoni kesi juu ya hilo. hatu uchunguzi wa jambo hilo haujawekwa wazi hata siku moja.
 lakini kuna kutekwa kwa DR Ulimboka  na kupigwa kwa Mwandishi wa habari  Absalom kibanda. matukio yote haya tunasikia mivutano ya polisi na wansiasa na pengine kutupa vichwa vy habari katika magazeti. je wananchi tufikiriea nini juu ya haya mabo.?
 tukiachia hayo tunakumbuka mabomu ya Mbagara na Gogo la Mboto hakuna taarifa tumepata, mabomu yaliyopigwa Arusha na baada kutumia nguvu za polisi kutumika katika mazishi ya waanga wa tukio hilo.
lakini ukiangalia matamshi ya viongozi wetu utaona kabisa kuna hatari mfano sio muda mrefu tulimsikia waziri mkuu kaiwatangazia polisi na vyombo vya usalkama kuwa " wapigeni tu"
sasa mambo kama haya yanatupa wasiwasi wananchi wakawaida.

No comments:

Post a Comment