Kume kuwa na mijadala mingi sana kuhusu amani hapa tanzania ambayo kimsingi lengo lake limeendelea kuwa ajenda ya wale wanojadiliana. suala hili limekuwa kwa mara nyingi likihusishwa na mitizamo ya kisiasa, dini, kabila , na mali.
lakini suala la kujiuliza amani inasababishwa na nini? kwa hali ya kawaida hakuna nafsi inayokuwa na amani kama haijaridhika. mfano mdogo ni pale unapokuwa na shida ya namna yoyote nafsi yako inakosa amani, na tumezoea kuwa tunatumia maneno haya "jambo hili linaiigharimu nafsi yangu, linanyima amani". maneno haya maana yake ni sawa na hali ya unafsi kutoridhika.
nafsi kimsingi huwa inakuwa na shida zake kama yenyewe inapokuwa peke yake yaani haina washiriki wengine wa nafsi kama hile. lakini inapokuwepo au zinapokuwepo nafsi nyingine mara nyingi zinaridhika kwa kuwa na misingi ya vitu vya pamoja. mfano mnaweza mkasema kuwa nafsi zetu zitaridhika pale wote tukapo kuwa tumesinzia, basi sote tutatakiwa kusinzia ili turidhishe nafsi zetu na kuwa na amani.
Mkisha kuwa na muungano huo sasa mnakuwa na nafsi ya umoja ambayo ni jamii na nafsi za jamii zinaridhika pale misingi ya jamii inapotekelezwa na kuonekana inatekelezwa. Na msingi mkubwa wa jamii ni usawa sio wa kila mtu bali wa kila mwana jamii kutegemeana na ridhiki ya wanjamii wengine. hivyo msingi wa kuridhika hautakuwa utashi wa mtu bali ridhaa ya mtu kwa misingi hile.
hivyo kama jamii imekubaliana usawa, utu, umoja, ubinadamu na misingi mingine ya hivyo basi jamii hiyo haitakuwa na amani mpaka misingi hiyo itekelezwe na ionekane kabisa inatendeka. na pengine vinaweza kutokea vikundi vingine vyenye nguvu na pengine visivyo na nguvu na kuanza kugombana ili kurudisha hali ya kuridhiki kwa nafsi zao.
lakini pia kama vikundi hivyo vitatumia nafsi hiyo kutengeneza jamii nyingine ambayo kimsingi haikuwa misingi ya eneo lile basi vitatengeneza vita nyingine ambayo itavitaka kuwa na nguvu ili kuleta misingi mipya.
hivyo utakuwa wajibu wa kila mwanjamii husika kutunza misingi hile ya kuridhisha nafsi za jamii ambayo ndiyo msingi wa amani ya jamii hiyo. na matokeo yake ni amani.
No comments:
Post a Comment