katika mijadala inayoendelea sasa juu ya rasimu ya katiba ya tanzania ni umwamba na ubabe lakini pia yapo mawazo yenye msingi kabisa ambayo wannchi wanhitaji kuyasema lakini mimi leo nataka kujadili umwamba unaendelea katika rasimu hii.
wapo wanaojadili haya kwa umwamba tu kuwa tunataka sisi tuitwe tanganyika na wengine tunataka sisi tuitwe zanzibar, huu ni umwamba tu kwa sababu msingi wa majina ni ule ujinga wa kuwa nikiitwa fulani ndo watu huko nje watniona mimi mjanja kweli. hivi mfano mtoto ukimbatiza jina la juma ikatokea mtoto huyo akabadilisha jina hilo je mtoto huyo ataacha kuwa mwanao?
sasa kusema tunataka tanganyika au zanzibar ni kutaka uvifua hasa wa wansiasa na walevi wachache. kimsingi jina tanganyika ni mazalia ya ukoloni na zanzibar vile vile. sasa ukibadilisha mhaya na mkurya na mjita wataacha kuoleana, mamni ataacha kunywa mbege, au mpemba ataacha kuvua samki. ili suala kwa kweli halina maana yoyote. nakumbuka mwalimu nyerere aliwa kudokeza kuwa "mipaka ya afrika haina maana" vivyo hivyo majina ya matifa ya afrika hayana maana pia.
naomba niishie hapo kwa leo ila mjadala huu sioni kama unamsingi sana kwa taifa
No comments:
Post a Comment