Mjadala wangu leo naona huwe kuhusu rasimu ya katiba mpya ya tanzania mabaraza na mijadala imeanza kwa kasi sana japo macho yaliyomengi yamejikita katika suala la muungano, hasahasa namba ya serikali wengine wakipendekeza serikali tatu, mbili, mkataba (bado sijajua nini maana ya mkataba), na serikali moja au kuvunja kabisa muungano.
Naona mjadala wangu ujikite katika masuala ya muungano lakini katika namna ya pekee kidogo. nianze na ibara ya 62(2) na (3) vifungu hivi vinahusu mahusiano ya kikanda na kimataifa.
ibara ya 62 (2) inasema bila kuathiri mipaka iliyowekwa na katiba hii , kila mshirika wa muungano atakuwa na uwezo na uhuru wa kuanzisha mahusiano na ushirikiano na jumuiya au taasisi ya kikanda na kimataifa kwa mambo yaliyo chini ya mamlaka yake kwa mujibu wa katiba ya mshirika wa muungano.
62(3) inasema : mshirika wa muungano anaweza wakati wa kutekeleza majukumu yake chini ya ibara ndogo ya (2), kuomba mashirikiano kutoka serikali ya muungano kwa ajili ya kufanikisha mahusiano na jumuiya au taasisi ya kikanda au kimataifa, na serikali ya jamhuri ya muungano inaweza kutoa ushirikiano kwa mshirika huyo kwa namna itavyohitajika.
kimsingi vifungu hivi vina maneno ambayo yanutata na maneno yayoweza kumfanya mshirika wa muungano kufanya mambo yake yeye mwenyewe anvyo jua kwa sababu maneno yaliyotumika haya mbani mshiriki huyo. mfano unaposema "anweza" na "inaweza" maneno haya haya mlazimishi mshirika yeyote kubanwa na kifungu hiki labda kumruhusu kufanya analoweza. Pengine kuomba ushauriano utatengemea busara za mshirika wa muungano.
pili vifungu hivi vinaingilia mambo ya muungano mfano " suala la mambo ya nje ni la muungano" unaporuhusu mshirika kuwa na mahusiano au mashirikiano maana yake huko utakuwa na watu wawili wa naoliwakilisha taifa moja. kwa sababu pia mambo ya nje ni pamoja na mahusiano ya kibiashara, kiimani, kimisaada na mikopo ya kimataifa. mfano nchi mshirika wa muungano inataka kuanzisha ubalozi na ukaona kuwa jambo hili serikali ya muungano italizuia basi mshirika huyo atakuwa tiyari kuomba ushirikiano, sasa katika hali kama hii itakuwa na mabalozi wawili. au mshirika antaka kuwa na kiti katika umoja wa mataifa na akungwa mkono na matifa mengine huko nje basi mshirika huyo atataka kuomba ushirikiano kutoka muungano.
suala hili ukiliangalia kwa namna nyingine utaona kabisa lisipoangaliwa litavunja muungano kwa sababu matifa mengine huko nje wanweza kuzitambua serikali za washirika kama matifa kamili suala linalo sabbisha double sovereignty na pengine itategemea na ni nani aliye tambua serikali hiyo anweza aktengeneza over sovereignty.
kwa kutambua uwepo wa urafiki na ujirani mwema sipingi serikali za washirika kuwa na marafiki au majirani ila sasa napendekeza maneno yaliyotumika yabdilike na yawe na hali ya kumlazimisha mshirika wa muungano kupata ridhaa ya serikali ya muungano kabla hajafanya mahusiano au mashirikiano ya kikanda na kimataifa.
SOMA KWA UDANI NA UONE LAKINI PIA UPITIE KWA UNDANI MASUALA YA MSINGI HAYO
ReplyDelete