Monday, 30 September 2013

kufungia vyombo vya habari ni kufisha demokrasia.

Demokrasia ni utawala shirikishi kwa ufupi yaani ni mfumo au muundo wa utawala unaotegemea sana uwazi,usawa, uwajibikaji, haki za binadamu na serikali inayoongozwa na wananchi wenyewe kupitia wawakilishi wao. Kimsingi suala la ushiriki wa wananchi linajikita katika maoni ya wananchi na taarifa kwa wananchi.

Na utawala wa kidemokrasia unategemea vyombo vya habari ndivyo viwe chachu ya taarifa kwa wananchi na kwa serikali kutoka kwa wananchi. kwa msingi huo vyombo vya habari vinawajibu wa kukusanya, kuchunguza na kutoa taarifa kwa wananchi na vivyo hivyo kutoka kwa wananchi kwenda kwa serikali. mfano chombo cha habari kinaweza kutafiti habari za hatari kwa dola zilizo kwa wananchi na kupeleka kwa dola au kutoka kwa dola dhidi ya wananchi.

kwa msingi huo suala la uwazi na kuheshimu maoni ya watu, pamoja na haki ya kupata habari vinakuwa ndio msingi mkuu wa demokrasia. dola lolote lile linawajibu wa kuhakikisha vyombo vya habari hivi vinafanya kazi katika misingi ya usawa bila kupendelea makundi ya watu fulani ndani ya jamii.

sasa nikizungumzia ufingiwaji wa vyombo vya habari hapa tanzania zikiwemo redio, na magazeti vimekuwa vikwazo vikubwa vya kufisha haki hiyo ya kidemokrasia na utawala bora. kwani inaonesha wazi kuwa ufungiwaji huu unakuwa mara nyingi ukilenga kuwanyima wananchi taarifa ambazo kimsingi wanahitaji kuzipata.

jambo hili linafisha demokrasia nchini na kusababisha watu kuwa katika mazingira ya woga na wasi wasi.

No comments:

Post a Comment